Hapo chini kuna link ya tovuti kutoka Idara ya Afya ya Ohio (Ohio Department of Health) inayoonyesha ramani ya vituo vya kupimwa gonjwa la COVID-19. Vituo vya serikali vinaonyeshwa na rangi ya bluu na vituo vya biashara binafsi vinaonyeshwa na rangi ya njano. Kuna maduka mengi ya dawa na supermarkets nyingi ambazo pia ni vituo vya kupimwa COVID-19. Kwenye ramani, tumia upande wa kulia kuchagua wilaya (county) yako kutafuta vituo vilivyo karibu na wewe.

 

https://coronavirus.ohio.gov/wps/portal/gov/covid-19/testing-ch-centers/

 

Muda siyo mrefu kutakuwa na vituo vya kupimwa gonjwa la COVID-19 mjini Cleveland. Tunatarajia Gavana wa Ohio atatoa taarifa kuhusu hivyo vituo na mahali vitakapokuwa wiki ijayo.