Jiliinde Dhidi ya Utapeli wa Virusi vya Corona

Wanaofanya utapeli mara nyingi wanatumia njia hizi zifuatazo kuomba hela:

  • Money Wire ambayo ni namna ya kutuma hela kwenye benki yaani unapewa namba ya akaunti ya benki ya mtu anayeomba hela pamoja na namba yake ya routing halafu unatuma kwa akaunti hiyo hiyo kupitia benki au shirika kama Western Union.
  • Hela ya mtandaoni kama bitcoin
  • Gift cards ambazo ni kadi zinazotumika kwenye duka moja.

Usitume hela kwa mtu akikuomba kwa njia hizo. Ofisi za serikali, makampuni ya teknolojia, pamoja na makampuni ya huduma (yaani gesi, maji, maji machafu, na umeme) hayatatumia njia hizo.

Tapeli za Kawaida:

Mara nyingi watu wanaofanya utapeli huwa wanataka hela yako au maarifa yako ili wakuibie. Mara nyingi wanafanya utapeli kama:

  • Matoleo ya hela kukusaidia kulipia bili
  • Matishio ya kukukamata au kuchukua akaunti zako za benki
  • Matoleo ya kukupatia vipimo, matibabu, au chanjo ya virusi vya corona
  • Mawasiliano kutoka polisi, IRS, au mashirika ya serikali

Usitoe namba yako ya Social Security ao namba za akaunti za benki kwa mtu yeyote!

Ishara za Kazi Danganyifu

  • Mwajiri anakuambia kuweka cheki kwenye benki halafu utume hela kwa mtu
  • Anakuomba kufungua akaunti ya benki au hela ya mtandaoni kwa ajili ya kampuni
  • Anakuambia kupokea hela au kulipia chochote kwa kutumia njia ya money wire, gift cards, au hela ya mtandaoni.
  • Anakuomba kupokea au kutuma tena barua au kifurushi

Ukiwa na shida ya utapeli, au unafikri unaona mtu anafanya utapeli, pigia simu namba ya Idara ya Mambo ya Minunuzi wilaya wa Cuyahoga (Cuyahoga County Consumer Affair): (216) 443-7226 au mtandaoni consumeraffairs.cuyahogacounty.us