Madabiliko ya Idara ya Biashara Ndogo (Small Business Administration au SBA)

Small Business Administration (SBA) inatafuta wafanyakazi wa muda mfupi wanaoongea lugha zaidi ya moja kusaidia na programmu za misaada ya Covid-19. Ajira zinazofanyika nyumbani zinapatikana hapa: https://www.sba.gov/page/disaster-response-jobs-sba

Aina za kazi zinazopatikana:

  • Mwanasheria, wakili, au wasaidizi wa kisheria – hata kama wewe ni mwanfunzi wa sheria na unasubiri matokeo ya mtihani wa bar
  • Mhuduma kwa wateja – ajira nzuri kwa wanafunzi wa biashara au fedha
  • Mtaalumu wa mikopo ya SBA
  • Msaidizi wa mikopo ya SBA
  • Msaidizi wa programmu za SBA

Tangazo: Uwezo mpya kuomba mikopo isaidiayo na matatizo ya kiuchumi (Economic Injury and Disaster Loan and Advance au EIDL na EIDL Advance). SBA itaanza kupokea maombi mapya ya mikopo ya EIDL na EIDL Advance yanayotoka biashara za kilimo za kimarekani

  • Biashara za kilimo ni zile zinazohusika uzalishaji wa chakula na nyuzi, ufugaji, kilimo cha samaki au mimea ya maji, na shuguli zote za kilimo zinazoandikwa katika sehemu 18(b) ya Sheria ya Bishara Ndogo (Small Business Act (15 U.S.C. 647(b)).
  • SBA inasisitiza biashara zote za kilimo zisizozidi wafanyakazi 500 na zinzazotaka kuomba mikopo hiyo zianze kuandaa maarifa zote zitakazohitajika.

Omba mkopo wa EIDL na EIDL Advance hapa

Mikopo ya PPP bado inapatikana! Itafute hapa: https://www.sba.gov/paycheckprotection/find