CLEVELAND METROPOLITAN SCHOOL DISCTRICT

UHESABIWE

CMSD Shindano la Sensa

Video za wanafunzi zinazosambaza taarifa ya sensa

CMSD inasisitiza umuhimu wa sensa ya mwaka 2020 na inataka wanafunzi wasaidie kusambaza umuhumu wake

Pamoja na Sherika la Cleveland (The Cleveland Foundation), shule ya CMSD inaomba wanafunzi wa chekechea hadi kidato cha 12 watengeneze videos zinazotia moyo watu wajaze fomu ya sensa

Wanafunzi 12 watashinda zawadi ya kadi ya visa ya dola $200

Watu wote wakishiriki na sensa itasaidia mahali watu wanapoishi, kama mje wa Cleveland, kupata hela kutoka serikali kuendana na idadi ya watu kwa ajili ya vitu kama huduma za umma. Lakini chini ya nusu ya idadi ya watu wanaoishi mjini Cleveland wamejaza sensa na tuko nyuma sana na miji mingine huku Ohio katika kujaza sensa.

Video za wanafunzi zinatakiwa zisizidi dakika moja na zieleze umuhimu wa sensa kwa familia zao na wasisitize marafiki zao, ndugu zao, na majirani wao kujaza sensa.

Wanafunzi wanaruhusiwa kuimba, kucheza musiki, kuandika, kurap, kuchora, au kufanya kitu chochote kinachosambaza ujumbe wa umuhimu wa sensa. Kuingia kwenye shindano, kwanza wanafunzi na familia zao zinatakiwa kuweka video zao kwenye akaunti zao za kijamii kama YouTube, TikTok, Instagram, Facebook, and Twitter. Usisahau kuweka tag ya #CMSDCounts au #inthistogetherOhio

Halafu itakubidi kufuatilia tovuti hii kuingiza video yako kwenye shindano: https://tinyurl.com/CMSDCensus kabla ya 11:59 PM, tarehe tano mwezi wa sita siku ya ijumaa.

Kamati ya Sensa ya CMSD itachagua washindi waliotumia ubunifu sana na waliofanikiwa kusambaza ujumbe wa sensa vizuri. Washindi wataambiwa kama wameshinda tarehe 12 mwezi wa 6. Kutakuwa na washindi wanne katika kila kikundi cha umri. Vikundi vya umri vitakuwa kwanzia chekechea hadi kidato cha 4, kidato cha 5 hadi kidato cha 8, na kidato cha 9 hadi kidato cha 12.

CMSD na masherika mengine mjini Cleveland yatatumia video za wanafunzi kusisitiza watu kujaza sensa.

Kwa taarifa zaidi au kwa maswali uliyo nayo, tuma barua pepe kwa [email protected]

Sensa inajazwa kwa urahisi mtandaoni, kwa simu, au kwa barua. Sheria za marekani ziansema kwamba taarifa zako binafsi zote zinatumika kwa usalama. Ukitaka taarifa zaidi kuhusu sensa, ingia kwenye tovuti ya www.2020Census.gov au pigia simu nambari hii ya sensa 844.330.2020

Mwongozo wako wa Sensa ya mwaka 2020/ Somali Language Guide