Idara ya Marekani ya Forodha na Uhamiaji (USCIS) imetoa miongozi mipya ya program ya DACA kuendana na maaumzi ya Mahakama Kuu tarehe 4 mwezi wa 12 mwaka 2020. 

Kwanzia tarehe 8 mwezi wa 12 mwaka 2020, ofisi ya USCIS itaanza kufanya vitu vifuatavyo: 

  • Itapokea maombi ya mara ya kwanza kwa program ya DACA kuendana na sera za DACA kabla ya tarehe 5 mwezi wa 9 mwaka 2017 
  • Itapokea maombi ya kuanzisha tena ushiriki kwenye program ya DACA kuendana na sera za DACA kabla ya tarehe 5 mwezi wa 9 mwaka 2017 
  • Itapokea maombi ya “advanced parole”, yaani uwezo wa watu wakiwa katika program ya DACA kusafiri nje ya Marekani na kurudi bila kupoteza ushiriki katika program ya DACA kuendana na sera za DACA kabla ya tarehe 5 mwezi wa 9 mwaka 2017 
  • Itaongeza muda ya program ya DACA iwe miaka miwili badala ya mwaka mmoja 
  • Itaongeza muda ya ruhusa ya kufanya kazi kwenye program ya DACA iwe miaka miwili badala ya mwaka mmoja 

Unaweza kuona ustahiki na uwezo wa kuomba program ya DACA hapa: https://www.uscis.gov/i-821d 

Ustahiki wa program ya DACA: 

  • Umekuwa chini ya miaka 31 tarehe 15 mwezi wa 6 mwaka 2012 
  • Umekuja Marekani kabla hujakuwa na umri wa miaka 16 
  • Ulikuwepo Marekeani tarehe 15 mwezi wa 61 mwaka 2012 pamoja na siku ulipoomba kujiunga na program ya DACA 
  • Ulikuwa hujatambuliwa kisheria nchini Marekani tarehe 15 mweziwa 6 mwaka 2012 
  • Unasoma sasa, umehitimu shule ya sekondari au umepata GED, au umemaliza mkataba ya kijeshi kwenye Coast Guard au Armed Forces 
  • Hujapata jinai au makosa madogo ya sheria na hujakamatwa