- Chanjo ya COVID-19 ni chanjo salama yenye mafanikio mazuri ya 94%
- Huwezi kupata ugonjwa wa COVID-19 kutoka chanjo ya COVID-19. Chanjo ya COVID-19 haina virusi hai, kwa hivyo huwezi kupata ugonjwa wa COVID-19 kupitia chanjo.
- Majaribio ya chanjo ya COVID-19 yalikuwa makubwa kuliko yote duniani. Kwa kawaida utafiti kuhakikisha ubora wa chanjo unakuwa na watu kama 5,000 ila jaribio la Modera lilikuwa na watu 30,000 na jaribio la Pfizer-BioTech lilikuwa na watu 40,000
- Chanjo za COVID-19 hazisababishi matatizo ya kiuzazi. Hakuna uthibitisho kwamba watu wliopata chanjo ya COVID-19 wanapata shida za kiuzazi
- Haikuwa na changamoto kubwa wakati wa majaribio ya chanjo ya COVID-19. Kuna dalili zinazotokea kwa kawaida kwa watuo wanochanjwa kwa COVID-19, lakini siyo dalili kubwa sana. Dalili za kawaida zinafanana na dalili za chanjo zingine kama uchovu, maumivu ya kichwa, na maumivu ya misuli
- Chajo za COVID-19 hazitabadilisha DNA au vinasaba vyako. Chanjo haziwezi kubadlilisha DNA ya mtu
- Chanjo hazina teknolojia yoyote ya ufuatiliaji. Hakuna teknolojia yoyote ya ufuatililaji au udhibithi kwenye chanjo ya COVID-19
- Chanjo hazisababishia usonji au tawahudi. Kuna utafiti unaoendelea duniani unaonyesha kwamba hakuna uhusiano kati ya usonji na chanjo ya COVID-19
